Timbulo Ft Jux – Nashukuru [Mp3 Download]

0

Timbulo Ft Jux – Nashukuru [Mp3 Download].

Timbulo X Jux – Nashukuru [Mp3 Download].

Click To Download

Related Songs

Msanii ambae kwa sasa anatamba na kibao cha nakumiss miss Timbulo amefunguka na kusema kuwa aliamua kuacha kazi yake ya ualimu wa shule ya msingi kwa sababu ya muziki,Timbulo amesema hayo leo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya jumatano kuanzia saa sita mchana mpaka saaa nane mchana.

Timbulo amesema kuwa yeye ni mwalimu ambae alisomea fani hiyo na pia ameifanya kazi hiyo kwa muda flani kabla ya kuamua kuipiga chini baada ya kuingia katika muziki na kuweza kufanikiwa,na sababu kubwa msanii huyo anasema imempelekea kuiacha kazi hiyo ni pamoja kipato duni katika fani yake hiyo.

‘Ni kweli mimi ni mwalimu na niko na vyeti vya ualimu lakini kwa sasa nimepumzika kufundisha na kufanya muziki kwa kuwa muziki unalipa zaidi ukilinganisha na kazi ya ualimu ambayo awali alikuwa akiifanya”

Timbulo ambae alianza kufanya vizuri katika bongo fleva na wimbo wake wa Domo langu amesema kuwa katika muziki wake hategemei kollabo ili kufanya vizuri kwani alianza muziki na kufanikiwa bila kollabo hivyo hadhani kama Kollabo ndiyo inaweza kumsimamisha mbali na kipaji na uwezo binafsi wa msaniii.

“Nilianza kutoka na niling’aa bila kollabo na nimeendelea kustiki katika game kwa muda wote huo bila hata kolabo, fuatilia ujue zaidi muzuki ni kipaji na uwezo wa mtu binafsi,unaweza fanya kollabo na msanii mkali ila kama kipaji huna huwezi fanikiwa”

NJE YA MUZUKI
Imezoeleka watu wengi kufanya kitu tofauti na kazi anayoifanya katika lengo la kuongeza kipato na kuendesha maisha ya kila siku hivyo msanii Timbulo amefunguka na kusema kuwa hata yeye mbali na kazi yake ya sanaa kwa sasa amekuwa akijushugulisha na biashara ili kukuza kiapato chake na kuendesha maisha yake nje ya kazi ya muziki,na hapo ndipo baadhi ya mashabiki walitaka kujua aina ya biashara anayofanya huku wengine wakisema kuwa huenda na yeye anajishugulisha na biashara ya kuuza poda kama ambavyo wasananii wengine wamekuwa wakihusishwa na biashara hiyo.

“Mimi ni mfanyabishara nje ya muziki wangu na kazi yangu ya ualimu lakini katika maisha yangu sijawahi hata siku moja kufanya biashara ya kuuza unga kama mnavyohisi au kama mnavyodai kuwa wasanii ndiyo kazi yetu hiyo,so hakuna ukweli katika hili”

MAPENZI YANALIPA ZAIDI
Msanii Timbulo amesema kuwa sababu kubwa wasanii wengi Tanzania na duniani kiujumla kuimba nyimbo za mapenzi sababu ndizo nyimbo zinazopendwa na kukubarika vizuri kwa wasikilizaji na ni rahisi kuteka hisia za wasikilizaji na watazamaji kwa kuwa ndiyo maisha wanayoishi kila siku.hivyo kila msanii atajitahidi kuona anawafurahisha mashabiki wake kwa kuwapa kazi nzuri ambayo wataipenda.

WAKIHITAJI MSAADA WANGU NITAWASAIDIA
Timbulo amefunguka na kusema kuwa kwa wasanii ambao walikuwa wakifanya vizuri na wameshindwa kupenya katika muziki kutokana na mambo mbalimbali ikitokea wakihitaji msaada wake katika jambo lolote lile atakuwa tayari kusaidiana nao ili kuweza fanikisha malengo yao katika suala lao.

“Wanamuziki wenzangu ambao kwa sasa hafanyi vizuri tena katika sanaa ikitokea wakihitaji msaada wangu niko tayar kuwasaidia katika jambo ambalo litakuwa ndani ya uwezo wangu”